Pages

Monday, April 20, 2015

HABARI KWA UFUPI




Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameitaka jumuiya ya albino nchini kuisukuma Serikali ili Rais Jakaya Kikwete asaini utekelezaji wa hukumu ya kuwanyonga wauaji wa albino.Kauli ya Lowassa imekuja wiki moja tu baada ya Rais Kikwete kusema hajapelekewa majina ya watu 16 waliohukumiwa kifo kutokana na mauaji ya albino kutokana na mlolongo mrefu wa kisheria uliopo kabla ya kumfikia.


Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Buni Ramole anayewania Ubunge Jimbo la Moshi Mjini, juzi alitinga mkutanoni na helkopta inayomilikiwa na Mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema).Ramole alitua na usafiri huo saa 10.37 jioni katika viwanja vya Pasua mjini hapa.

Chama cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimemfukuza uanachama Mwanasiasa Mkongwe Hassan Nassor Moyo baada ya kubainika amekuwa akifanya vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya chama ikiwamo kuhutubia mikutano ya hadhara inayoitishwa na Chama cha Wananchi (CUF) na kukejeli misingi ya Mapinduzi na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar imefahamika visiwani humo jana.

Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi ametoa wito wa kufanyika kikao cha dharura cha viongozi wa umoja wa ulaya kujadili swala la wahamiaji wanaoangamia kwenye bahari ya Meditarenean wakijaribu kuingia ulaya. Inafuatia ajali ya hivi punde ambao karibu watu 700 wanahofiwa kufa maji baada ya boti kuzama baharini kaskazini mwa Libya, kilomita 200 kutoka kisiwa cha Lampedusa, nchini Italia.

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema inavoelekea dawa ya kuuwa magugu ndio chanzo cha vifo vya watu 18 vilivyotokea kusini-magharibi mwa Nigeria, bila ya sababu kujulikana.Katika siku chache zilizopita wakaazi katika jimbo la Ondo wamekufa saa chache baada ya kuhisi macho hayaoni sawasawa na kuumwa na vichwa.

No comments:

Post a Comment