Pages

Wednesday, April 13, 2016

HABARI KWA UFUPI




Siku moja baada ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Anne kilango kuvuliwa uongozi kwa kutosema ukweli,Mkuu wa wilaya ya kishapu Hawa Nghubi ameiruka taarifa ya kutokuwepo kwa watumishi hewa ambayo amesema ilimshtua alipoiona kwenye televisheni.


Ripoti ya utafiti kuhusu ujangili wa meno ya Tembo imebaini kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi mbili za Afrika ambazo idadi kubwa ya Tembo wanauawa.Utafiti huo wa njia ya vinasaba (DNA)uliofanywa na shirika la umoja waMataifa ya kupambana na Dawa za kulevya na uhalifu(UNODC),Benk ya Dunia (WB)na Shirika la polisi la Kimataifa (Interpol)ulibaini kuwa asilimia 85 ya meno ya tembo yanayokamatwa asilia yake ni mbuga za Selous,Ruaha na Ruangwa, Tanzania.

Waasi nchini Sudan Kusini wanasema kuwa wanachama wake 16 wa kitengo cha habari, wamekamatwa na kupigwa vibaya na maafisa wa usalama katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba.Kundi hilo la waandishi wa habari lilikuwa limetanguliwa katika mji mkuu wa Juba, siku kadhaa kabla ya kuwasili kwa kiongozi wa waasi Dkt Riek Machar.

Mawakala kutoka afisi ya mkuu wa sheria nchini Panama wamevamia jengo la kampuni ya mawakili ya Mossack Fonseca, kutafuta ushahidi wowote unaohusiana na biashara haramu.Kampuni hiyo imeshutumiwa kwa kuepuka kulipa kodi na ulaghai lakini mwanzilishi wake Ramon Fonseca amesema kuwa operesheni zake zote ni halali.

Muungano wa ulaya umelaani hatua ya rais wa Macedonia, Gjorge Ivanov, kuwasamehe wanasiasa waliohusishwa na ufisadi.Kamishna anayehusika na upanuzi wa muungano huo Johannes Hahn, amesema kuwa msamaha huo hauambatani na uelewa wake wa sheria na hivyo, unahatarisha azma ya Macedonia kuwa mwanachama wa muungano huo.

No comments:

Post a Comment