Meli yenye abiria 460 ikizama Korea Kusini
Oparesheni ya uokozi inaendelea kufuatia ishara za
dharura zilizoripotiwa kutoka meli moja iliyobeba takriban abiria 460
katika pwani ya Korea Kusini.
Maafisa wanasema kuwa walinzi wa pwani hiyo
wanatumia, meli za wanamaji wa Korea pamoja na ndege za uokoaji
kuwaokoa watu waliokuwa katika meli hiyo.
Shughuli zinaendelea hivi sasa kuokoa zaidi ya abiria 460 wa ferry hiyo .
Jeshi la wanamaji likishirikiana na maafisa
wanaolinda usalama katika bahari ya rasi ya Korea wanasema watu wengi
wamefanikiwa kuolewa.
Maafisa wanasema walipokea habari kuwa meli hiyo
imepata matatizo ikiwa imebeba idadi kubwa ya wanafunzi ikitoka Incheon
iliyoko kwenye visiwa vya kifahari vya Jeju .
Waokoaji wamewanusuru tayari abiria 160 huku wengine waliosalia wakishauriwa waruke baharini iliwaokolewe.
Walioshuhudia wanasema kulisikika kishindo kikubwa kabla ya ferry hiyo kuanza kuzama zaidi ya kilomita 20 kutoka ufukweni.
Shughuli ya uokoaji bado inaendelea.BBC
No comments:
Post a Comment