Makundi ya wanaharakati wanaoiunga mkono Urusi yameteka
majengo ya Serikali
Marekani imeelezea wasiwasi mkubwa kuhusu mzozo
unaozidi kutokota mashariki mwa taifa la Ukraine ambapo makundi ya
wanaharakati wanaoiunga mkono Urusi yameteka majengo ya serikali na
kutangaza baadhi ya majimbo katika eneo hilo kuwa Jamhuri.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani
John Kerry ameionya Moscow kuwa kutakuwa na adhabu iwapo itaendelea na
hila ya kuivuruga Ukraine.
Bwana
Kerry alimwambia mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov kuwa utekaji wa
majengo ya umma ulionekana kupangwa kikamilifu katika miji mitatu
Mashariki mwa Ukraine.
Alisema utekaji nyara huo ulionekana kuchochewa
kwa ushirikiano na Serikali ya Urusi na akasisitiza kuwa mipango zaidi
ya kuvuruga amani nchini Ukraine itasababisha kuwepo kwa masharti makali
zaidi kuwekewa Urusi vikwazo zaidi.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Marekani, Jay Carney
alisema kuwa mawaziri hao wawili walishauriana kuhusu kupanga mkutano
kati ya Ukraine, Urusi, Marekani na Ulaya. Jay Carney alizungumza mjini
Washington ambapo aliwambia waandishi wa habari kuwa hatua yo yote
itakayochukuliwa na Urusi katika maeneo hayo ya Ukraine ni kinyume cha
sheria.
‘Watu hawa hawana mamlaka yo yote ya kisheria
kuchua hatua hizo. Ikiwa Urusi itaingia Mashariki mwa Ukraine, kwa njia
moja au nyingine hali itakuwa mbaya zaidi. tunatoa wito kwa rais putin
na serikali yake kusitisha hatua zote za kuvuruga ukraine.’
Mashauriano kati ya Bwana Kerry na Bwana Lavrov
yanaendelea wakati Ukraine inapozidi kuwatuma maafisa wa usalama zaidi
katika miji ya Mashariki ya Donetsk, Luhansk na Kharkiv kufuatia utekaji
wa majengo ya Serikali na makundi yanayounga mkono utawala wa Urusi.
Katika Donetsk, watu walioshikilia jengo la
Utawala wametangaza wanachotaja kama "Jamhuri ya wananchi". Katika picha
za video zilizonaswa na mmoja wa mashahidi wa tukio hilo na
kupeperushwa na runinga ya Ukraine, mtu ambaye hakutambuliwa anasikika
akisema kuwa Jamhuri iliyojitangaza itauliza Urusi iwatume wanajeshi
katika eneo hilo iwapo Ukraine itapinga upigaji wa kura ya maoni.BBC
No comments:
Post a Comment