Nahodha wa meli iliyozama Lee Joon Seok
Viongozi wa mashitaka nchini Korea Kusini wameiomba
mahakama kutoa kibali cha kukamatwa kwa nahodha wa feri ya abiria
iliyozama siku ya Jumatano ikiwa imewabeba zaidi ya watu 400.
Hadi kufikia sasa watu mia mbili na sabini hawajulikani waliko.
Jitihada za kutafuta karibu abiria mia mbili hamsini waliokuwa kwenye feri hiyo zinazidi kukumbwa na changamoto.
Wapiga mbizi wanaojaribu kuingia ndani ya chombo hicho walifanikiwa
kuingia eneo la mizigo lakini wakashindwa kuyafikia maeneo mengine
Mmoja wa wapiga mbizi hao alisema kuwa hawakufanikiwa kuiona vizuri feri hiyo hali iliyowalazimu kuiguza kwa mikono yao.
Afisa wa ulinzi wa pwani Ko Myung Suk amesema kuwa hawakupata manusura yeyote eneo walilofanikiwa kufika
Naibu mwalimu mkuu kwenye shule ambapo wengi wa wanafunzi walikuwa wakisomea amepatikana ameaga dunia.
Vyombo vya habari vinasema kuwa huenda mwalimu huyo amejitoa uhai.Bbc
No comments:
Post a Comment