Pages

Tuesday, June 03, 2014

HABARI KWA UFUPI




Harakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 zimeanza. Polisi wameanza mafunzo yatakayowaongezea uwezo wa kusimamia uchaguzi huo.Mafunzo hayo yanafadhiliwa na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kupitia mradi wake wa Uwezeshaji wa Demokrasia (DEP).


Wakazi wa maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam jana walikumbwa na taharuki baada ya kituo cha daladala cha Mwenge kuhamishiwa eneo la Makumbusho .Mwananchi lililokuwa kwenye kituo hicho mapema jana, lilishuhudia baadhi ya abiria wakistaajabu hali ya mabadiliko hayo ambayo yalipokewa kwa shangwe na wakazi wa Makumbusho huku wale wa Mwenge wakipingana na uamuzi.

Msanii muigizaji kutoka Kenya Lupita Nyong'o ameteuliwa kuijiunga na mabingwa wengine wa kimataifa katika filamu maarufu zaidi duniani STAR WARS.Lupita anatarajiwa kuonekana katika kipindi cha saba msimu huu wa Star Wars.

Polisi nchini katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja wamepiga marufuku maandamano ya watu wanaowaunga mkono zaidi ya wasichana wa shule mia mbili waliotekwanyara na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali za kiislamu la Boko Haram mwezi Aprili.

Zaidi ya wakimbizi 130,000 kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo wamefukuzwa kutoka Congo Brazaville tangu mwezi Aprili.Wengi wao sasa wanaishi katika kambi za muda nchini DRC.

No comments:

Post a Comment