Pages

Monday, May 19, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI



Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza anadaiwa kuhamisha gari la wagonjwa kutoka Kituo cha Afya cha Kibiti kwenda Zahanati ya Nyamisati kwa ‘shinikizo la wakubwa’.Gari hilo lililotolewa na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) kwa Kituo cha Afya Kibiti kwa ajili ya kusaidia wakazi wa maeneo hayo na jirani, lakini Mahiza aliagiza lihamishiwe Nyamisati ambako inadaiwa wanatoka “watu wazito wenye ushawishi mkubwa”.


Bomu lililolipuka katika mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria limewaua watu 5 na kuwajeruhi wengine wengi.Shambulio hilo limefanywa katika eneo linaloaminiwa kuwa na waumini wengi zaidi wa dini ya kikristu, ambao wamekuwa wakilengwa mara nyingi na wapiganaji wa Boko Haram.

Tahadhari zaidi zimetolewa nchini Kenya za kutokea mashambulio katika baadhi ya maeneo ya umma na foleni za barabarani.Mitandao ya kijamii ya twitter na face book imetumiwa kusambaza ujumbe miongoni mwa wananchi kutoa tahadhari hiyo.

Serikali ya Libya imesisitiza kuwa bado imedhibiti uongozi wa nchi.Hii ni hotuba ya kwanza kutoka kwa serikali hiyo tangu kutokea mapigano katika mji mkuu Tripoli siku ya Jumapili.Maafisa wanasema kuwa watu 2 wameuawa na wengine zaidi ya 55 kujeruhiwa katika mapigano hayo ambayo ni ya punde zaidi.

No comments:

Post a Comment