Pages

Saturday, May 17, 2014

40 WAUAWA KWA SHAMBULIZI BENGHAZI


                                Waziri mkuu wa Libya Abdallah Al Thinni amekuwa akisisitiza 
                                 kuwa Serikali haikuamuru kuhusu shambulio hilo

Wizara ya afya nchini Libya imesema zaidi ya watu 40 wameuwawa mjini Benghazi siku Ijumaa katika mashambulizi anga na nchi kavu yaliyoongozwa na kanali wa zamani wa jeshi dhidi ya wanamgambo wa kiislam.


Vurugu hizo zilizofanyika zinaelezwa kuwa zilikuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea tangu mapinduzi ya yaliyomuondoa madarakani Kanal Muamar Gadafi mwaka 2011.

Taarifa kutoka mjini Benhgazi zinasema hivi sasa utulivu umerejea kwenye mji huo kama ilivyokuwa awali.
Mtu aliyeogoza mashambulizi hayo, Khalifa Haftar amesema ataendelea na kampeni yake ya kuwaondoa watu wote aliowaita magaidi nje ya mji wa Benghazi.

Serikali kuu imelaani matumizi hayo ya nguvu na kuuita hatua hiyo kama jaribio la mapinduzi lililoshindwa.BBC

No comments:

Post a Comment