Pages

Thursday, March 13, 2014

NDEGE WA AJABU



Ndege wa ajabu wanaosadikiwa kutoa kinyesi chenye sumu kali,wamevamia kisiwa cha musira kilichopo Manispaa ya Bukoba na kusababisha vifo vya mifugo kama ndege  anaofugwa,huku ukali wa sumu hiyo ukisababisha kutoboka mabati ya nyumba zilizopo kisiwani humo.

Ndege hao wanaoaminika kuvamia kisiwa hicho mwezi mmoja uliopita tayari wamesha sababisha vifo vya kuku 516 na mbuzi 12 wanaodaiwa kula au kugusa kinyesi chao.Hata hivyo bado haijafahamika ndege hao wanatokea nchi gani.

Akithibitisha habari hizo mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe anasema serikali ilipata taarifa hizo kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya na baadaye kuundwa timu ya kutafuta taarifa za awali za tatizo hilo.

Massawe alisema pamoja na ndege pamoja na kusababisha vifo vya mifugo na ndege wafugwao pia baadhi ya miti katika kisiwa hicho imekauka na mabati kutoboka inapotokea kinyesi chao kitaangukia kwenye paa za nyumba zao.

No comments:

Post a Comment