Pages

Monday, May 12, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI



Siku moja baada ya mmoja kati mawaziri wanaotajwa kuwa mizigo, Christopher Chiza, kupata wakati mgumu kupitisha bajeti ya wizara yake ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoundwa na wabunge wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),
imepania kukwamisha bajeti ya Wizara ya Maji, inayoongozwa na waziri mwingine mzigo, Profesa Jumanne Maghembe.

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imehamasisha jumuiya ya wafanyabiashara nchini kuchangamkia fursa za biashara katika Umoja wa Mataifa (UN).Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, katika semina ya kuwahamasisha wafanyabiashara wa Tanzania kufahamu na kuzitumia fursa za biashara zinazojitokeza UN.

Serikali imekiri kupoteza mabilioni ya fedha kila mwaka ambazo zinapaswa kulipwa kwa mujibu  wa  sheria na makampuni ya migodi nchini kama ushuru wa huduma kwa halmashauri  zinazozunguka migodi hiyo.Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, alieleza hayo mwishoni mwa wiki wakati alipozungumza na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Tarime, mkoani Mara baada ya kukabidhi hundi ya dola 800,000 za Marekani (sh bilioni 1.3) ambazo zimetolewa na mgodi wa North Mara kama deni la mrahaba kwa Halmashauri ya Tarime.

Chama cha Waganga wa Tiba Asili Nchini (ATME), Mei 15, mwaka huu kinatarajia kukutana na wahariri 40 kutoka vyombo mbalimbali vya habari kwa ajili ya kuwapa semina juu ya huduma ya tiba hiyo.Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa ATME Taifa, Boniventure Mwalongo, alisema wameamua kukutana na wanataaluma hao kama njia mojawapo ya kufikisha yale yote muhimu yanayohusu afya na tiba asili, ili hatimaye yaweze kuwafikia wananchi.

Saa chache tu baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa usitishaji mapigano nchini Sudan kusini Malumbano yameibuka .Sasa Serikali na wapiganaji wa Sudan Kusini wanalaumiana kila upande ukimshutumu mwenzake kuvunja makubaliano hayo yaliyosainiwa ijumaa.Hata hivyo kiongozi wa waasi Riek Machar anasema bado ameazimia kutekeleza makubaliano hayo licha ya kwamba anasema serikali ya rais Salva Kiir inavunja mapatano hayo.


Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.

No comments:

Post a Comment