Pages

Monday, May 12, 2014

AUKATA ULIMI WAKE HEKALUNI ILI APOKEE BARAKA KWA MUNGU WA WAHINDI




Kijana wa miaka 17,ameukata ulimi wake vipande vipande kwa  kisu na kuuweka hekaluni kama tendo kubwa la   ibada kwa Mungu wake wa wahindi maarufu Lord Shiva.

Lalmohan Soren akiwa katika hekalu laMahedevgarha huko Dugda Jharkhand nchini India alitekeleza azma yake na waumini wa hekalu hilo walipofika asubuhi kwa ajili ya kuabudu wwalikutana na damu zilizokuwa zimetapakaa chini.
Ulimi wa Lalmohan ulikuwa ndani ya bakuli karibu na miguu yake huku miguu yake huku kukiwa na nakaratasi kinachosemwa “Nimekata ulimi wangu kama sadaka kwa Mungu Shiva tafadhali msinitoe  nje ya hekalu,mimi nataka niendeleekukaa hapa chini ya ulinzi wa Mungu “
Kiongozi mara baada ya kupata taarifa alifanikiwa kumshawishi Lalmohan kwenda hospitali.
Madaktari walijaribu kurudisha na kuutengeneza upya ulimi wake kwa kuushonea sehemu aliyokata na kisu kikali ilishindikana na hivyo kumruhusu arudi nyumbani baada ya siku chache.
Eneo hilo la makabila ya Santhal nchini India ni maarufu sana kwa matukio ya ajabu ambayo yanaaminika kama ni ya kishirikina ambao watu huufanya katika kuiomba miungu yao.

No comments:

Post a Comment