Pages

Tuesday, March 24, 2015

HABARI KWA UFUPI




Rais Jakaya Kikwete amelikata Jeshi la Polisi nchini kujiandaa kikamilifu ili kukabiliana na vurugu zozote zitakazojitokeza wakati wa uandikishaji wapigakura, upigaji Kura ya Maoni ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu.


Mwanamuziki mwenye uwezo na mvuto jukwaani, Juma Nature amesema kuwa hana mpango wa kugombea ubunge katika Jimbo la Temeke mwaka huu, licha ya awali kutangaza nia hiyo.Nature ametoa kauli hiyo huku wasanii wengine wakitangaza nia ya kuwania ubunge majimbo mbalimbali.

Wakati joto la mbio za kuwania urais likiendelea kuisisimua nchi, Umoja wa Wanawake Wanasiasa Tanzania (Ulingo), kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba, umesema tayari wameandaa majina matano ya wanawake kuwania nafasi hiyo baadaye mwaka huu.

Waziri mkuu wa Uingereza, hataendelea tena na wadhfa wake huo, iwapo atarudi madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwezi Mei.David Cameron, ameiambia BBC kuwa, anadhani awamu ya tatu inaweza kuwa ni kipindi kirefu kwake kukaa madarakani na kiongozi mpya ni vizuri kuchaguliwa.

Raisi Barack Obama ametoa mwito kwa wa Nigeria kusitisha vurugu hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mapema mwishoni mwa wiki hii.Wasi wasi wa hali ya usalama umezidi kuongezeka nchini humo wakati siku ya kupiga kura kadiri inavyokaribia ambapo wananchi wa Naijeria wanatarajiwa kupiga kura jumamosi wiki hii baada uchaguzi huo kuhairishwa mwezi uliopita kutokana na mashambulio ya kundi la Boko Haram.

No comments:

Post a Comment