Pages

Friday, March 20, 2015

HABARI KWA UFUPI



Pamoja na mpango wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuliaga Bunge kukwama jana, Chama cha ACT- Tanzania kimetangaza kukamilisha maandalizi ya kumpokea mwanasiasa huyo kuanzia leo.


Serikali imeombwa kuingilia kati mgogoro unaoendelea baina yake na nchi jirani ya Kenya, kuhusu kuzuiliwa kwa magari ya Tanzania ya kusafirisha watalii kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata ili kuleta usawa na ustawi wa sekta ya utalii kwa nchi zote mbili.

Rais Obama ametoa ujumbe katika kanda ya video kwa viongozi na raia wa Iran akisema kwamba hapajakuwa na wakati muafaka zaidi katika miongo kadha iliyopita kwa Marekani na Iran kutafuta uhusiano mpya.

Uingereza imesema itasaidiana na Kenya katika kukabiliana na makundi ya kigaidi ili kuboresha amani kama njia bora ya kukuza uhusiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond amesema hayo baada ya Kenya na Uingereza kutia saini mkataba wa maelewano baina ya mashirika ya biashara na viwanda vya nchi hizo mbili.

Rais Obama amemtumia salaam za pongezi waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kutokana na ushindi uliokipata chama chake katika uchaguzi uliofanyika Jumanne.Lakini Bwana Obama ameelezea dhamira yake ya kuupatia ufumbuzi mgogoro kati ya Israel na Wapalestina kuwa ni kuunda taifa la Palestina.

No comments:

Post a Comment