Pages

Thursday, September 11, 2014

HABARI KWA UFUPI



Makubaliano baina ya Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kutaka Bunge Maalumu lifikie ukomo Oktoba 4, mwaka huu yamezua sintofahamu mjini hapa huku uamuzi huo ukionekana kuwachanganya viongozi wa Bunge hilo.


Rais Jakaya Kikwete jana aliwafukuza makada wa CCM waliokuwa wakimsubiri kwenye kituo cha dharura cha ebola alipokitembelea kwa kushtukiza katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameamuru mabango ya hekeheka za uchaguzi yenye nembo ya kauli mbiu ya 'Bring Back Jonathan 2015' yang'olewe mara moja.

Liberia inakabiliwa na tisho kubwa kwa utaifa wake huku janga la Ebola likiendelea kuenea kwa kasi kubwa nchini humo.Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya waziri wa ulinzi nchini humo.

Wafungwa wawili wamepigwa risasi walipokuwa wakijaribu kutoroka kutoka katika mahakama moja nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment