Pages

Friday, July 04, 2014

HABARI KWA UFUPI



Siku mbili baada ya Kaimu Balozi wa Libya, Ismail Nwairat kujiua kwa risasi akiwa ofisini kwake, Jeshi la Polisi kupitia kikosi maalum cha uchunguzi wa matukio ya kujiua, limeanza uchunguzi wa kifo hicho.


Watu wasiofahamika wamemuua mkazi wa Kijiji cha Vikonge Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi,  Kitola Jeremia (45) kwa kumkatwa mapanga sehemu za mwili wake sambamba na kumtoboa tumbo .

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amewataka wakulima wazungu waliosalia nchini humo kuondoka na kuwaachia mashamba wazalendo wa nchi hiyo.Chama cha wakulima wazungu, kimesema kuwa matamshi ya Mugabe yanasikitisha sana na kwamba taharuki ya kibaguzi imeanza kutanda.

Mwanamke mmoja aliyemtelekeza mwanawe ndani ya karatasi ya plastiki katika bustani moja nchini Uingereza aponea adhabu ya kifungo jela.Mtoto huyo mchanga aliyekuwa wa siku moja tu, alipatwa na mtu aliyekuwa anamtembeza Mbwa wake katika bustani hilo.

Polisi nchini Uganda wamedhibiti usalama mjini Kampala kufuatia onyo la mashambulizi ya kigaidi kupangwa kufanywa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe.Maafisa wa usalama katika uwanja huo, walisema kuwa onyo la shambulizi hilo lililopangwa kufanyika Alhamisi linapaswa kuchukuliwa kwa uzito.

No comments:

Post a Comment