Pages

Wednesday, March 25, 2015

SHUGHULI YA UOKOAJI ZIMEANZA TENA UFARANSA



                                          Ndege za uokoaji zimerejelea shughuli

Polisi nchini Ufaransa wameeleza kuwa hali mbaya ya hewa itakwamisha zoezi la utafutaji miili ya watu wapatao mia moja na hamsini katika eneo la ajali ya ndege na hivyo kuchukuwa siku kadhaa.

                                              Hali ya anga imeathiri uokoaji

Siku ya jana ndege ya Ujerumani ilianguka katika eneo la milima ya Alps huko Ufaransa na kuua watu wote wapatao mia moja na hamsini waliokuwemo.

Waathirika wa ajali hiyo wanatoka nchi mbali mbali ambapo arobaini na tano ni wahispania huku zaidi ya sitini wakiwa ni wajerumani.

Kumi na sita, kati yao walikuwa ni wanafunzi kutoka shule moja nchini Ujerumani ambao walikuwa wakijerea kutoka katika ziara ya kutembelea Hispania.
                                    Hali ya hewa katika Milima ya Alps nchini Ufaransa

Pierre-Henry Brandet msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani amewaambia waandishi wa habari kwa zoezi la kuuopoa na kutambua miiili ndio kinachoopewa kipau mbele.

"Kipaumbele chetu ni kupata miili mingi kwa kadri tuwezevyo ili kuwafanya wataalam wa utambuzi wa uhalifu waweze kuifanyia utambuzi.
                                Jamaa na marafiki ya walioathirika wakitoa rambirambi zao

Na sio miili pekee kitu chochote ambacho kitatusaidia kuitambua miili kama vile mizigo ya abiria ambayo atakuwa ameibeba itachukuliwa na itatuwezesha kuupeleka mwili katika nchi aliyotoka lakini ni mapema kusema ni wakati gani."
                                                               Ndege za uokoaji

Naye Raisi wa Marekani Barack Obama amesema kwamba taifa lake linaungana na mataifa ya Ujerumani na Hispania katika kipindi hiki kigumu walichopoteza wapendwa wao."Nataka kusema kwamba mawazo na sala zetu tunazielekeza kwa marafiki zetu walioko Ulaya ,na hasa kwa watu wa nchi za Ujerumani na Hispania ,kufuatia ajali mbaya ya ndege iliyotokea nchini Ufaransa.

Utafutaji miili ukiendelea

Inaumiza kwa sababu ajali hiyo imepoteza watoto wengi kwa wakati mmoja ,na walio wengi watoto wachanga.nilimpigia simu kansela wa Ujerumani Angela Merkel natarajia kuongea na Raisi ama waziri mkuu wa Hispania Rajoy baadaye leo kutoa salamu za rambi rambi kutoka kwa watu wa Marekani ,lakini pia kutoa msaada wowote utakao hitajika wakati huu wa uchunguzi wa chanzo cha ajali iliyosababisha janga kubwa.."BBC


No comments:

Post a Comment