Pages

Monday, March 30, 2015

HABARI KWA UFUPI




Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema, amemsamehe Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye hivi karibuni alimtolea maneno makali kutokana na kutofautiana naye juu ya msimamo wa viongozi wa Kikristo kuhusu Katiba Inayopendekezwa.


Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ametoa wito kwa vijana barani Afrika kupinga dhana ya ukoloni mamboleo pamoja na kulinda rasilimali zilizopo ndani ya bara hili kwa masilahi ya vizazi vijavyo.Rais Mugabe alitoa kauli hiyo juzi, wakati akizindua kongamano la tatu la viongozi vijana Afrika linalofanyika hapa na kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki 400 kutoka China na Afrika.

Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo ifikapo Jumatatu jioni.Upigaji kura uliendelea katika siku ya pili ya uchgaguzi baada ya kutokea hitilafu katika kadi za kielektroniki na kuchelewesha usajili wa baadhi ya wapiga kura.

Idara ya usalama nchini Brazil imesema kuwa imewaua watu saba waliokuwa wakifanya jaribio la kupora katika benk moja na ambao pia wanadaiwa kujihusisha na dawa za kulevya.Taarifa hizo zinasema kuwa majambazi hao walianza kurushiana risasi na Polisi katika mji wa Novos Kaskazin Mashariki mwa Brazil.

Mazungumzo kuhusu mpango tata wa Iran wa nyuklia yameendelea nchini Uswisi, kwa kuwasili mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa sita yenye nguvu duniani.Kiongozi wa mazungumzo wa Iran Abbas Araqchi amesema makubaliano yanawezekana-- lakini mazungumzo yako katika hatua ngumu na bado kuna mambo ya kutatua.

No comments:

Post a Comment