Pages

Thursday, March 26, 2015

HABARI KWA UFUPI




Rais Jakaya Kikwete na mwenzake Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi wamezindua safari za treni tatu za mizigo ‘block train’ kutoka Dar es Salaam kwenda Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).


Jeshi la Polisi mkoani Simiyu linawashikilia askari wawili wa magereza na polisi kwa kukutwa na noti bandia ikiwa pamoja na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Charles Mkumbo alisema askari hao walikamatwa juzi saa tisa mchana katika Mtaa wa Old Maswa, Kata ya Nyakabindi, wilayani Bariadi.

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema kuwazuia wananchi kwenda nyumbani kwake kumshawishi agombee urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu ni sawa na kuzuia mafuriko kwa mkono.Lowassa alitoa kauli hiyo nyumbani kwake mjini Dodoma jana wakati alipotembelewa na kundi jipya kutoka Mbarali mkoani Mbeya waliokwenda kumshawishi atangaze nia kugombea urais.

Ubalozi wa Marekani nchini Uganda, umesema una taarifa za uwezekano wa shambulio la kigaidi nchini humo.Aidha Marekani pia imetoa tahadhari kwa raia wake.Taarifa ya ubalozi huo umebainisha kwamba shambulio hilo linaweza kutekelezwa wakati wowote, katika maeneo ambayo raia wa mataifa ya Magharibi na Marekani hukutana.

Saud Arabia imeanza operesheni zake za kijeshi nchini Yemen, ikiwa ni kujibu ombi la Rais wa nchi hiyo Abd Rabbuh Mansour Hadi.Balozi wa Saudi Arabia Nchini Marekani amesema kuwa, taifa lake na washirika wao wa ghuba wanatumia mashambulizi ya angani katika harakati za kuunga mkono serikali halali ya Yemen, ili isichukuliwe na kundi wa waasi la Houthi.

Wakaguzi wa kifaransa wamesema wamefanikiwa kukipata kifaa cha kurekodia sauti na maneno kutoka katika kisanduku cheusi cha ndege ya shirika la ndege la ujerumani iliyopata ajali katika milima ya Alps.Wakaguzi hao mpaka sasa wanaendelea kukitafuta kisanduku kingine ,ambacho hurekodi taarifa za ndege hiyo na chanzo cha ajali hiyo . Timu hiyo ya uokozi iliyoko katika eneo la ajali lililoko upande wa Kusini mwa Ufaransa wamefanikiwa kukipata kifaa hicho kinachohifadhiwa katika chumba cha rubani kikiwa kimeharibika.

No comments:

Post a Comment