Pages

Thursday, March 20, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI




Baadhi ya wasomi na wachambuzi wa masuala ya kisiasa hapa nchini wamesema hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadilko ya Katiba, Jaji  Joseph Warioba itasaidia kubadilisha msimamo wa wajumbe wengi wa Bunge Maalumu la Katiba.

Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba katika Bunge hilo tayari kwa kuijadili, kuiboresha na hatimaye kutoka na Rasimu ya Tatu itakayopigiwa kura ya ama kuikubali kuwa Katiba Mpya au la.
                                   ***************************
Majibizano makali yameshuhudiwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo mataifa mengi yameshutumu uamuzi wa Urusi kunyakua eneo la Crimea,kilele hatahivyo ilikuwa majibizano makali baina ya mabalozi wa Marekani na Urusi.
                                   ****************************
Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sudan Kusini na waasi wanaoongozwa na aliyekuwa naibu wa rais wa nchi hiyo Riek Machar yanatarajiwa kuanza tena leo mjini Addis Ababa Ethiopia.Mazungumzo hayo yaliahirishwa mapema mwezi huu baada ya mazungumzo ya hapo awali kukwama.
                                   ****************************
Mahakama kuu nchini Kenya imepinga agizo la kutokamatwa kwa mwandishi Walter Baraza baada ya wakili wake Kibe Mungai kushindwa kufika mahakamani ili kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Hatua hiyo inamaanisha kwamba waziri wa usalama nchini Kenya Joseph Ole Lenku anaweza kuomba agizo la kukamatwa kwa mwandishi huyo kabla ya kuwasilishwa katika mahakama ya ICC anakotakikana.

No comments:

Post a Comment